Mwamama Mbishi ambaye huwa anapenda changamoto za Kimaisha Asha Baraka
"Iron Lady" Ameanza harakati zake za kuwania nafasi ya kuingia Bungeni
mwaka 2015 kwa tiketi ya chama cha mapinduzi kwenye Wilaya mpya ya
Uvinza.
Wilaya hii ya Uvinza ni zao la Iliyokuwa Wilaya ya Kigoma Vijijini baada
ya kugawanywa mara mbili na kuwa Kigoma Kaskazini na Uvinza. Jimbo la
Kigoma Kaskazini kwasasa linashikiliwa na Mheshimiwa Zubery Zitto Kabwe
ambaye kwasasa ameshatamka bayana kuwa anakusudia kugombea Uraisi kwa
tiketi ya Chama chake cha CHADEMA hivyo hatagombea tena Ubunge kwenye
Jimbo lake hilo la Kigoma Kaskazini. Aidha Mheshimiwa David Kafulila
Mbunge machachari kutoka Chama cha NCCR Mageuzi ambaye alikuwa kwenye
sakata la kupingana na Mwenyekiti wa Chama Chake Mheshimiwa Mbatia hadi
kufikia hatua ya kufukuzwa uanachama na Sakata hilo kusimamishwa
uanachama kwa kile kilichoitwa Usaliti wa Chama.
Mama Asha Baraka katika kuhakikisha kuwa anaweka mambo yake vizuri awamu
hii aliamua kwenda kugombea ujumbe wa NEC kupitia chama Chake cha CCM
mkoani Kigoma Ngazi ya Wilaya ya Uvinza kufuatia utaratibu ambao chama
hicho umejiamulia baada ya ule wa ngazi ya Kitaifa. Awali mama Asha
baraka alikuwa mjumbe wa NEC kupitia Kapu la akina mama lakini kwasasa
amekuwa Mjumbe wa NEC baada ya kushinda uchaguzi huo jana Wilayani
Uvinza kwa jumla ya Kura 322 kati ya 590 zilizopigwa na kuwaacha wapinzani wake wawili wakigawana kura 268 zilizosalia.
Uchaguzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Red Cross Kigoma mjini
ndani ya chumba ambacho kilikuwa na Vumbi jingi kwakuwa bado jengo hilo
halijakamilika. Bibi Asha Ramadhani Baraka aliwaomba wasimamiaji wa
uchaguzi kumtoa nje ya ukumbi huo kutokana na matatizo ya afya yake
ambayo kwa kawaida yeye ana ATHIMA ugonjwa ambao hauhitaji hewa Chache.
Kutokana na taratibu za uchaguzi ilikuwa ni vigumu kumruhusu kutoka nje
ili asije akaharibu matokeo ambayo yalikuwa bado hayajatangazwa. Idadi
ya watu waliokuwa katika chumba hicho kidogo ilikuwa ni Polisi watatu,
wagombea watatu na wasimamizi wa uchaguzi watatu, hivyo ilikuwa ni
vigumu kwa wajumbe kupata hewa ya kutosha hali iliyopelekea Asha Baraka
kuzidiwa baada ya kukosa Pumzi.
Asha Ramadhani Baraka baada ya Kupoteza Fahamu kwa kukosa pumzi |
Msimamizi wa Uchaguzi aliamuru Asha Baraka akimbizwe Hospitali ya Mkoa
Maweni na mara alipofika hapo alichomwa sindani AMINOFLINE na kurejea
katika hali yake ya kawaida. Hadi matokeo yanatanazwa Asha Baraka
alikuwa Hosiptalini lakini alijawa na furaha baada ya kusikia kuwa
amechaguliwa kuwa Mjumbe wa NEC kwa kura 322 na kuwashinda Wapinzani
wake.
Akiongea kwa simu kutoka Kigoma Asha Baraka ametamba kuwa sasa nguvu
zake nyingi sasa anazielekeza zaidi kwa kwenye kukijenga Chama chake
Wilayani Uvinza na amejipanga vema kuhakikisha Mwaka 2015 kama Mungu
akimuweka hai kupambana na Mbunge wa sasa David Kafulila.