UTANGULIZI
Iliripotiwa
kupitia vyombo vingi vya habari kuwa
nilianguka ghafla na kupoteza fahamu nilipokuwa nikishiriki katika uchaguzi wa
C.C.M katika ngazi ya Wilaya mpya ya Uvinza
Mkoani Kigoma.
Mara
baada ya kutangazwa kwa habari zile, ziliniletea usumbufu mkubwa kwangu mimi
mwenyewe pamoja na ndugu zangu wa karibu kwa kupokea simu mara kwa mara
zilizokuwa zikitaka kujua ukweli wa taarifa.
UKWELI
ULIVYO.
Nilichukua
fomu kwa ajili ya kugombea Ujumbe wa NEC ya C.CM kupitia Wilaya mpya ya Uvinza
iliyoko Mkoani Kigoma. Mara baada ya kipindi cha Kampeni kumalizika, ilifika
wakati wa uchaguzi ambao ulifanyika siku ya Jumapili tarehe
30-09-2012.
Mara
baada ya kumalizika kwa taratibu zote za uchaguzi ulifika wakati wa kupokea
matokeo, wakati taratibu za upokeaji matokeo zikiendelea, nilianza kuhisi dalili
ya PUMU (ATHMA) kunizidia kutokana na kukosa hewa kulikosababishwa na udogo wa
chumba kilichokuwa kikitumika kwa ajili ya shughuli hiyo, nilimuomba Msimamizi
wa Uchaguzi ruhusa ya kutoka nje ili nipate nafasi ya kupata hewa nzuri lakini
Msimamizi wa Uchaguzi kwa vigezo vya taratibu za uchaguzi wa C.C.M na kutokujua
kama ni mwenye matatizo ya PUMU alinikatalia kutoka nje ya chumba.
Mara
baada ya kukataliwa nilitii maamuzi ya msimamizi na kuendelea kuivumilia hali ile mpaka
ilipokuwa mbaya kabisa nilimuomba tena msimamizi ili nitoke nje na alinikubalia.
nilipotoka
nje nilijilaza chini kwa kukosa nguvu na kwa kuwa nje palikuwa na watu wengi
walidhani nimezidiwa basi kila mtu alianza kutaka kunipa huduma ya kwanza wapo
walionivua viatu, wapo walionimwagia maji na wapo pia waliokuwa
wakinipepea.
nilipoona
hali ya taharuki imezidi ndipo nilipomuomba Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Uvinza
Mhe. Fatuma Nyembo usafiri ili nikachome sindano ya kutuliza PUMU ambayo ilianza
kunizidia.
Mara
baada ya kuchoma sindano nilirejea katika hali yangu ya kawaida kama hapo awali.
Ikumbukwe maradhi ya PUMU yamekuwa yakiniandama kwa muda mrefu sasa takribani
kwa miaka 13. Mara zote huwa inanizidia lakini nimekuwa nikichoma sindano na
kurejea katika hali yangu ya kawaida.
Pia
hali ya pumu kunizidia ilikuwa ni mara baada ya shuguli nyingi za kichaguzi za
ndani ya C.C.M kumalizika na kuibuka mshindi wa kwanza kwa kujizolea kura 322
huku nikimwacha mbali mpinzani wangu JOSEPHINE NAWEZA aliyepata kura
210.
Kutokana
na ushindi huo mimi sasa hivi ni mjumbe wa NEC kupitia wilaya ya Uvinza yenye
tarafa za Nguruka, Uvinza, Malagarasi, Sunuka, Kazuramimba, Kandaga, Ilagara,
Igalula, Sigunga, Bihungi, Kalya, Mtego wa Mti, Mganza na Itebula.
MWISHO
NA HITIMISHO.
Napenda
kutoa ahsante kwa wale wote walioguswa na mpaka kunitafuta kwa njia moja au
nyingine kutokana na habari hii na kuwajulisha kuwa mimi nipo imara kabisa na
ninaendelea na shughuli zangu kama kawaida na kwa sasa nipo bado
Kigoma.
AHSANTENI
ASHA
BARAKA (MNEC)
MKURUGENZI
WA ASET