Tuesday, October 16, 2012

MWANATANGA BLOGSPOT: ASHA BARAKA AJIPANGA KUMVAA DAVID KAFULILA 2015 JIMBO LA UVINZA KIGOMA

0 comments
MWANATANGA BLOGSPOT: ASHA BARAKA AJIPANGA KUMVAA DAVID KAFULILA 2015 JIMBO LA UVINZA KIGOMA


 


Mwamama Mbishi ambaye huwa anapenda changamoto za Kimaisha Asha Baraka "Iron Lady" Ameanza harakati zake za kuwania nafasi ya kuingia Bungeni mwaka 2015 kwa tiketi ya chama cha mapinduzi kwenye Wilaya mpya ya Uvinza. 
Wilaya hii ya Uvinza ni zao la Iliyokuwa Wilaya ya Kigoma Vijijini baada ya kugawanywa mara mbili na kuwa Kigoma Kaskazini na Uvinza. Jimbo la Kigoma Kaskazini kwasasa linashikiliwa na Mheshimiwa Zubery Zitto Kabwe ambaye kwasasa ameshatamka bayana kuwa anakusudia kugombea Uraisi kwa tiketi ya Chama chake cha CHADEMA hivyo hatagombea tena Ubunge kwenye Jimbo lake hilo la Kigoma Kaskazini. Aidha Mheshimiwa David Kafulila Mbunge machachari kutoka Chama cha NCCR Mageuzi ambaye alikuwa kwenye sakata la kupingana na Mwenyekiti wa Chama Chake Mheshimiwa Mbatia hadi kufikia hatua ya kufukuzwa uanachama na Sakata hilo kusimamishwa uanachama kwa kile kilichoitwa Usaliti wa Chama.
Mama Asha Baraka katika kuhakikisha kuwa anaweka mambo yake vizuri awamu hii aliamua kwenda kugombea ujumbe wa NEC kupitia chama Chake cha CCM mkoani Kigoma Ngazi ya Wilaya ya Uvinza kufuatia utaratibu ambao chama hicho umejiamulia baada ya ule wa ngazi ya Kitaifa. Awali mama Asha baraka alikuwa mjumbe wa NEC kupitia Kapu la akina mama lakini kwasasa amekuwa Mjumbe wa NEC baada ya kushinda uchaguzi huo jana Wilayani Uvinza kwa jumla ya Kura 322 kati ya 590 zilizopigwa na kuwaacha wapinzani wake wawili wakigawana kura 268 zilizosalia. 
Uchaguzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Red Cross Kigoma mjini ndani ya chumba ambacho kilikuwa na Vumbi jingi kwakuwa bado jengo hilo halijakamilika. Bibi Asha Ramadhani Baraka aliwaomba wasimamiaji wa uchaguzi kumtoa nje ya ukumbi huo kutokana na matatizo ya afya yake ambayo kwa kawaida yeye ana ATHIMA ugonjwa ambao hauhitaji hewa Chache. Kutokana na taratibu za uchaguzi ilikuwa ni vigumu kumruhusu kutoka nje ili asije akaharibu matokeo ambayo yalikuwa bado hayajatangazwa. Idadi ya watu waliokuwa katika chumba hicho kidogo ilikuwa ni Polisi watatu, wagombea watatu na wasimamizi wa uchaguzi watatu, hivyo ilikuwa ni vigumu kwa wajumbe kupata hewa ya kutosha hali iliyopelekea Asha Baraka kuzidiwa baada ya kukosa Pumzi.
Asha Ramadhani Baraka baada ya Kupoteza Fahamu kwa kukosa pumzi
Msimamizi wa Uchaguzi aliamuru Asha Baraka akimbizwe Hospitali ya Mkoa Maweni na mara alipofika hapo alichomwa sindani AMINOFLINE na kurejea katika hali yake ya kawaida. Hadi matokeo yanatanazwa Asha Baraka alikuwa Hosiptalini lakini alijawa na furaha baada ya kusikia kuwa amechaguliwa kuwa Mjumbe wa NEC kwa kura 322 na kuwashinda Wapinzani wake.
Akiongea kwa simu kutoka Kigoma Asha Baraka ametamba kuwa sasa nguvu zake nyingi sasa anazielekeza zaidi kwa kwenye kukijenga Chama chake Wilayani Uvinza na amejipanga vema kuhakikisha Mwaka 2015 kama Mungu akimuweka hai kupambana na Mbunge wa sasa David Kafulila.

Leave a Reply

Followers

 
UVINZA FM COMMUNITY RADIO © 2012 | Designed by Emmanuel Hilonga