Sunday, October 7, 2012

Faida Za UFM Radio

0 comments

Jamii ya Wilaya mpya ya Uvinza itafaidika na mengi zaidi ya kusambazia ujumbe kwa ujio kwa redio ya jamii - Uvinza FM Community Radio (UFM) , zifuatavyo ni baadhi tu ya faida :-

  • UFM itawapa sauti wakazi wa Uvinza hasa wazee na kundi la watu wenye hali ya chini ambao hawawezi kufikia vyombo vingine vya habari kupitia malumbano na kubadilishana mawazo ili kutoa hoja mbali mbali kwa kutumia lugha wanayoifahamu.
  • Jamii yote kujihusisha na miradi ya maendeleo kwa faida ya wote
  • Kupata elimu za stadi za maisha, ujasiriamali na habari ya mambo yanayoendelea duniani kote
  • Kupata elimu ya afya na mazingira
  • Kupata elimu ya ujana kwa vijana wote na kudumisha mila na desturi
  • Burudani tofauti kuzingatia watu wa rika zote
Kwa ujumla UFM redio itakua kama chanjo ya itakayoweza kupunguza magonjwa yanayozuilika, jawabu rahisi la kufikia malengo ya maendeleo, kuilinda Uvinza yetu tete isimong'onyoke kabisa, kufurahia na kutukuza mila na desturi zetu wana kimalampamba, kwa hiyo basi tutasema bai bai kwa maadui watatu wakubwa - magonjwa, umaskini na ujinga!

PAMOJA TUNAWEZA kuifufua Uvinza yetu!

Leave a Reply

Followers


 
UVINZA FM COMMUNITY RADIO © 2012 | Designed by Emmanuel Hilonga