Sunday, October 7, 2012

Airtel yashirikiana na UNESCO kuanzisha Radio

0 comments

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na UNESCO
wamejiunga kuendeleza sekta ya mawasiliano nchini na kuhakikisha
huduma za mawasiliano ya radio zinawafikia wananchi wengi hasa wale
wanaoishi kwenye maeneo ya vijiji zinavyokumbwa na changamoto
nyingi za kijamii pamoja na kukosekana kwa huduma za radio.
Airtel na UNESCO kwa kutambua umuhimu wa mawasiliano katika karne hii
ya 21 na katika kuhakikisha jamii inapata habari za uchumi, siasa na
za kijamii ambazo ndizo nyenzo muhimu kwa maendeleo ya jamii yeyote
duniani wameonelea ni vyema kwa kushirikiana na jamii husika kuanzisha
radio za jamii (community Radios) ili kutoa nafasi kwa wananchi kupata
elimu mbalimbali kwa kupitia Radio hizi zitakazoenea nchini kote.
Lengo kubwa la kuanzisha radio hizo ni kwasababu maeneo mengi yamekosa
huduma hizi muhimu za mawasilino na hivyo kujikuta kuwa kwenye mifumo
duni ya kijamii kama vile ukiketwaji wa wanawake, elimu duni, imani
za kishirikina, Umaskini , unyanyasaji wa kijinsia, kuenea kwa kasi
kwa ugonjwa wa ukimwi na matatizo mengine mengi.
Akiongea wakati walipotembelea Radio iliyopo Ololosokwani msimamizi wa
mradi na Afisa uhusiano wa Airtel bi Jane Matinde alisema, “Airtel
tunajisikia furaha kuwafikia wananchi na wateja wetu kwa kupitia
mtandao wetu uliompana zaidi,
tunaamini kwa kupitia radio hizi elimu itatolewa kwa jamii,
upatikanaji wa habari za kiuchumi na biashara kutawezesha kuboresha
shughulili za kiuchumi katika maeneo husika na nchi kwa ujumla, pia
radio hizi zitawapa wakazi kufahamu hali ya kisiasa nchini na kupata
habari mbalimbali za ndani na nje ya nchi tofauti na ilivyo sasa.
Airtel tunawajali sana na ndio maana ndio mtandao pekee unaopatikana
hapa kijijini Ololosokwani , na leo hii pia bado tumepiga hatua
nyingine kwa kushirikiana na wenzetu wa UNESCO kufikisha huduma ya
radio pekee ya Tanzania kijinini hapa ambayo masafa yake yatasikika
hadi vijiji vya jirani”
Airtel tunaendelea kutimiza dhamira yetu kwa kushirikiana na serikali
ya jamuhuri ya muungano chini ya wizara husika kuhakikisha tunachangia
katika kufikisha huduma hii muhimu kwa watanzania na kuleta mabadiliko
ya kiuchumi na kijamiii katika maeneo yanayoonekana ni duni na ambayo
hayajafikiwa.
Naye Afisa mradi wa habari na mawasiliano UNESCO Yusuph Al Amin
alisema” mradi wa radio hapa kijiji cha Ololosokwani utawawezesha
wakazi wa hapa kupata mawasiliano ya karibu na sehemu mbalimbali za
Tanzania, kutawawezesha kujifunza mambo mapya, kutangaza mila na
desturi za kimasai, kuweza kufahama mambo ya utawala bora na kuweza
kuhoji viongozi wao, kupata habari mbalimbali, na pia kuelimisha
wamasai kuendeleza tamaduni zao na maendeleo kwa ujumla.
“Tunawashukuru wenzetu wa Airtel kwa kushirikiana nasi katika
kuuanzisha mradi huu kwa kupitia radio hii tutaweza kufikia vijiji 14
pindi tutakapoanza kurusha matangazo”alisema Bw, Al Amin
Bw Al-Amin pia aliongeza kwa kusema “Pamoja na mradi wa radio pia
tumeweza kuanzisha multimedia center itakayowasaidi wakazi wa kijijini
hapa na shule ya sekondari iliyopokaribu kuweza kutembelea tovuti
mbalimbali na kuweza kupata huduma za internet”
Vile vile tumeanzisha mradi wa kuboresha nyumba zakimasai kuondoa
moshi na kuongeza mwanga na tutajenga nyumba mbili za mfano hivyo
tunategemea wakazi wa hapa watajenga nyumba za makazi zilizo na
kiwango kulinganisha na sasa na mradi mwengine ni wa kuboresha maziwa
ya ngome na nyama na kuweza kutengeneza viwanda vidogo na kutengeneza
jibini na mwisho tunaanzisha mradi wa solar utakao wawezesha wakazi wa
hapa kupata umeme” aliongeza Al Amin
Miradi yote hii imeanzishwa baada ya kuanza mradi wa radio na kuona
maeneo mengine ambayo tunaweza kuyaboresha na kuleta mabadiliko kwa
wakazi wa hapa alimalizia kwa kusema Bw, Al Amin
Akiongea na waandishi wa habari mkazi wa kijiji cha ololoskwani
aliyejitambulisha kwa jina la bi Nekisho Ndoinyo alisema hapa kijijini
kwetu hatuna radio ya Tanzania tuaamini kabisa kwa kuanzishwa radio
hii kutaleta mafanikio makubwa kwa vikundi vya kina mama na wakazi wa
hapa kutangaza biashara zao, tutaweza kupata taarifa mbalimbali ,
tutaweza kutangaza mila yetu ya kimasai, watoto wetu watapata elimu na
kuweza kujua nafasi mbalimbali za shule na kazi, hivyo basi nachukua
fulsa hii kuwahamasisha wanakijiji kushiriki katika vipindi vya radio
pale itakapoanza kurusha matangazo yake, tumefurahi sana kuweza kupata
mawasiliano haya ya radio na tunashukuru sana Airtel na UNESCO kwa
jitihada hizi.
Kwa upande wake mkazi wa kijiji cha ololosokwani bi Kootu Tome
aliongeza kwa kusema tatizo kubwa la kijiji hicho ni mgogoro wa Ardhi
na wawekezaji kuvamia maeneo yao hivyo naamini radio itatoa mwanga kwa
jamii na kuweza kutambua haki yao ya kimsingi.
Mradi huu wa Radio za jamiii unaosimamiwa na UNESCO kwa kushirikiana
na Airtel unategemea kufunguliwa rasmi mwishoni mwa mwenzi Juni kwa
kuzindua kituo cha Radio kilichopo Ololosokwani Arusha. Mikoa mingine
itakayofikishiwa radio za kujamii ni pamoja na Kyela Mbeya, Uvinza
Kigoma, Pemba na maeneo mengi.

Leave a Reply

Followers


 
UVINZA FM COMMUNITY RADIO © 2012 | Designed by Emmanuel Hilonga